Sunday, August 25

SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LATOA MSAADA WA VIFAA VYA OFISI KATIKA KITUO CHA HUDUMA SHUFA WILAYANI KAHAMA.

0MRATIBU WA MASUALA YA ULINZI WA MTOTO HAKI NA UTAWALA ALEX ENOCK KUTOKA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN KUSHOTO AKIMKABIDHI TV KAIMU MGANGA MKUU WA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA DR LUCAS DAVID.

   KAHAMA

Jamii wilayani Kahama mkoani Shnyanga imetakiwa kutumia kituo cha huduma Shufa (One Stop Center) kilichopo katika hospitali ya Wilaya ya Kahama ili kutoa taarifa za Unyanyasaji wa watoto na kina mama ikiwa ni pamoja na kupata msaada wa kisheria.

Wito huo umetolewa leo mjini Kahama na Mratibu wa masuala ya Ulinzi wa mtoto haki na Utawala Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children katika makabidhiano ya Vifaa vya ofisi hiyo yaliyofanyika katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Enock amesema Vifaa walivyotoa vina lenga kuongeza motisha kwa maafisa wa kituo hicho ikiwa ni sambamba na kutoa huduma bora kwa wateja ambao ni wahanga wa maswala ya ukatili wa kijinsia wilayani Kahama na maeneo jirani.
Akitaja vifaa walivyotoa Enock amesema ni pamoja na Viti,Kitanda cha wagonjwa,Tv,Meza,Mabenchi ya kukalia,Kabati pamoja na vifaa vya kuchezea watoto na kutoa wito kwa maafisa wa kituo hicho kuvitunza ili viweze kudumu muda wote wa Mradi.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii halmashauri ya mji wa Kahama Arinda Bwakeya amesema kuwa wanashukuru kupata msaada huo kwani utasaidia kuinua utendaji wao wa kazi na kwamba kituo hicho kimekuwa msaada mkubwa katika kupata taarifa nyingi za vitendo vya unyanyasaji.
Awali akipokea msaada  wa          vifaa hivyo Kaimu mganga mkuu halmashauri ya Mji wa Kahama Dr Lucas David amesema kuwa kituo cha huduma Shufa kimekuwa msaada mkubwa kwa jamii na kuongeza kuwa vifaa walivyopata watavitumia kwa kazi Iliyokusudiwa ili kutoa huduma bora kwa wateja wote wanaofika katika kituo hicho.
kituo cha huduma Shufa (One Stop Center) Cha wilayani Kahama mkoani Shinyanga kimeanzishwa mwaka 2016 kwa lengo la kuhudumia watu wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukatili wa watoto.

MATUKIO KATIKA PICHA:

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.