Thursday, August 22

SERIKALI YATOA SHILINGI MILIONI 700 KUSAIDIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA UKUNE HALMASHAURI YA USHETU.

0


 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA USHETU MICHAEL MATOMOLA

KAHAMA

Serikali imetoa shilingi milioni 700 kwa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama kwa lengo la kusaidia ujenzi  na ukarabati wa kituo cha afya Ukune  kata ya Ukune ili  kuimarisha huduma ya afya kwa wananachi  wa kata hiyo na kata jirani.
Akizungumza jana wakati wa kukagua shughuli ya ujenzi na ukarabati wa kituo hicho, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, MICHAEL MATOMORA, amesema shilingi milioni 400 zitatumika kwa shuguli za Ujenzi na shilingi milioni 300 ni kwaajili ya vifaa tiba.
Kukamilika kwa Ujenzi na  Ukarabati huo urapungumza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama  ambapo kwa mujibu wa MATOMORA, fedha hizo kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili wananchi wapate huduma  bora za afya ikiwamo upasuaji.
Wakati huo huo  benk ya CRBD imetoa hundi ya shilingi milioni 8 kwaajili ya ukamilishaji wa Zahanati ya Kijiji cha Ulowa ambayo boma lake lipo kwenye  hatua ya ukamilishaji.
Akikabidhi hundi hiya, Meneja wa benk ya CRDB, tawi la Kahama, LUTER MNENEY amesema benk hiyo itaaendelea kushiriki  na kuchangia katika shughuli za mbalimbali za  maendeleo katika kijamii.

 MATUKIO KATIKA PICHA:

 VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI WAKIKAGUA NYUMBA YA MGANGA KATIKA KATA YA UKUNE HALMASHAURI YA USHETU.

 UKAGUZI UKIENDELEA KATIKA JENGO LA WAHUDUMU WA KITUO CHA AFYA UKUNE
 MAFUNDI WAKIWA KATIKA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA KISASA KATIKA KATA YA UKUNE.
 VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI WAKIKAGUA NA KUPEWA MAELEKEZO KUHUSU UJENZI WA KITUO KIPYA CHA AFYA UKUNE.

 MBUNGE WA JIMBO LA USHETU ELIUS KWANDIKWA KULIA AKIWA NA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI WAKIKAGUA KITUO CHA AFYA UKUNE.

 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA USHETU MICHAEL MATOMOLA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUMALIZA UKAGUZI WA KITUO CHA AFYA UKUNE.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.