Thursday, August 22

NABII TITO KUPELEKWA MIREMBE NA MAHAKAMA

0


Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imemuamuru Mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka hospitali kuu ya magonjwa ya akili (Mirembe), mkazi wa kijiji cha Nong’ona Tito Onesmo Machibya maarufu kama (Nabii Tito), ili kuchunguzwa kama ana ugonjwa wa akili au la.

Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo James Karayemaha amesema anahitaji majibu hayo mnamo Marchi 5 mwaka 2018 siku ambayo mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani ikiwa ni baada ya agizo la mtuhumiwa huyo kupimwa akili kutotekelezwa hapo awali.

Nabii Tito Machibya alifikishwa Mahakamani hapo akituhumiwa kufanya uchochezi wa kidini kupitia mafundisho anayo yatoa na amekuwa akiieleza Mahakama kuwa amekuwa akifanya hivyo kwa sababu ana matatizo ya akili na kutoa vithibitisho toka hospitali ya Taifa Muhimbili.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.