Monday, August 19

MH KWANDIKWA AWAHAKIKISHIA WANANCHI UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA USHETU

0


Serikali imetenga shilingi bilioni 1.5 kwaajili ya ujenzi wa hosipitali ya  halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.
Akizungumza  na wakazi wa Kata ya ulowa, Naibu waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa alisema  tayari fedha hizo  zipo mbioni kutolewa  na serikali ambapo hadi sasa mchakato wa kuanza usanifu  wa  michoro ya majengo  kwaajili ya kuanza  kuinua maboma.
Alisema   kukamilika kwa ujenzi wa  hospitali ya Ushetu itasaidia kupunguza  changamoto ya wagonjwa kuetembea umbali mrefu kwenda hospitali ya  halmashauri ya Mji wa Kahama  kwani watakuwa wakipata matibabu kwenye hospitali  hiyo ambayo majengo yake yatakuwa ya kisasa.
Hata hivyo Naibu waziri Kwandikwa alisema  mbali na hilo, serikali imejipanga kuimaraisha sekta ya afya kwa kuboresha  vituo vya afya katika katta mbalimbali ambapo katika halmashauri ya Ushetu  wameanza kuboresha ujenzi wa kituo cha afya Ukune na watajenga  kingine kata ya Nyalwelwe.
Kwa upande wake Mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri ya Ushetu Michael Matomora alisema  hadi sasa wamepokea shilingi milioni 700, kwaajili ya upanuzi wa kituo cha afya Ukune na kwamba wameanza kuboresha zahanati ya Kijiji cha Ulowa..
Akizungumza na Kijukuu Blog Kaimu Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dokta Lucas David alisema  kukamilika kwa ujenzi wa hospitali za  halmashauri ya Msalala na Ushetu ni wazi kwamba itasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Halmashauri ya mji wa KAHAMA.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.