Monday, August 19

DC KAHAMA AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUWAFICHUA WAHALIFU MIGODINI.

0


 MKUU WA WILAYA YA KAHAMA FADHILI NKURLU AKIONGEA NA WACHIMBAJI WADOGO KATIKA SHEREHE YA UZINDUZI WA KAMPENI YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA UPANDAJI MITI KATIKA MGODI WA MWIME.

KAHAMA
Na William Bundala/Ndalike Sonda
Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imewataka wananchi waishio katika maeneo ya migodi migodo wilayani  humo kuhakikisha wanaripoti kwa vyombo vya ulinzi na usalama matukio yote yanayoashiria uvunjifu wa amani katika maeneo ya migodi  hiyo.
Akizungumza leo kwenye  uzinduzi wa  kampeni ya  ya utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti  katika  mgodi wa Kabela Ilindi Gold mine Mkuu  wa wilaya ya Kahama FADHILI NKURLU amesema kila mchimbaji wa madini anawajibu wa kulinda  usalama.
NKURLU amesema kutokana na wingi wa watu katika migodi midogo  ni lazima ulinzi na usalama uimarishwe pamoja na utunzaji wa mazingira kwa lengo  kuzuia magonjwa ya mlipuko huku akiupongeza uongzi wa Mgodi Kabela Ilindi kwa utunzaji wa mazingira na usalama.
Awali akisoma risala ya mgodi huo SHADRACK NYAMHOKYA, amesema  wavamimizi wa maduara wamekuwa wakileta hofu  juu ya usalama wa wachimbaji katika mgodi hu, huku wakiiomba serikali kuboresha barabara ya kutoka Mji Kahama kwenda kataka mgodi huo.
Katika    uzinduzi  wa kampeni ya  utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti katika Mgodi huo,NKURLU ameongoza zoezi la upandaji wa miti,  ambapo miche ya miti 500 imeoteshwa, huku  akiahidi kupeleka mingine elfu 10 katika mgodi huo.
MATUKIO KATIKA PICHA:

KIKOSI CHA MATARUMBETA KIKIONGOZA MAANDAMANO YA SHEREHE  YA UZINDUZI WA KAMPENI YA UTUNZAJI  WA MAZINGIRA NA UPANDAJI WA MITI MGODI WA MWIME KAHAMA

WANACHAMA WA KIKUNDI CHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KATIKA MGODI WA MWIME KAHAMA

BAADHI YA WAFANYAKAZI WA IDARA YA AFYA KATIKA MGODI WA MWIME KAHAMA WAKICHEZA KATIKA MAANDAMANO HAYO

GARI LA POLISI KAHAMA LIKIONGOZA MAANDAMANO YA SHEREHE HIZO.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA FADHILI NKURLU AKISALIMIANA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MGODI HUO.

WAFANYAKAZI WA KITENGO CHA USALAMA  NA UKAGUZI MGODINI HAPO  WAKIWA WAMESIMAMA KUPOKEA MAANDAMANO YA SHEREHE HIZO.

KIKOSI CHA USALAMA  NA UKAGUZI MGODINI HAPO WAKIWA WAMEMBEBA MAJERUHI  KWAAJILI YA KUMPA HUDUMA

MMOJA WA WASANII  ALIYEALIKWA KWAAJILI YA KUSHEREHESHA KATIKA SHEREHE HIYO

BAADHI YA WAFANYAKAZI WA IDARA YA AFYA MGODINI WAKIWA WANAELEKEA KWENYE ENEO LA KUKATA UTEPE KWAAJILI YA KUZINDUA UPANDAJI WA MITI MGODINI.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA FADHILI NKURLU AKIKATA UTEPE KWAAJILI YA UZINDUZI WA UPANDAJI WA MITI  MGODINI.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA FADHILI NKURLU AKIPANDA MITI MGODI WA MWIME

MATUKIO KATIKA PICHA YANAENDELEA……….Read More

Share.

About Author

Comments are closed.