Friday, July 19

WAZIRI JAFO AKABIDHI RASMI MASHINE MAALUMU ZA KUTIBU MAGONJWA MBALI MBALI KATIKA HOSPITALI YA KISARAWE

0


1

Waziri wa chi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kulia Selemani Jafo akikata utepe wakati wa sherehe ya kukabidhi mashine kwa ajili ya kutibu magonjwa mbali mbali katika hospitali ya Kisarawe, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo

2

Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia Jonathan Budenu akifafanua jambo kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo mara baada ya kukabidhi mashine hizo katika hospitali ya Wilaya.

3

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza na wananchi hawapo pichana pamoja na wauguzi na madaktari katika halfa ya kukabidhiwa rasmi mashine maalumu kwa ajili ya kutibu magonjwa mbali mbali katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe.

4

Waziri wan chi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kulia wakiwa na baadhi ya viongozi wengine wa serikali wa kati kati ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo na kushoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kisarawe Musa Gama katika halfa hiyo ya makabishiano ya mashine za kutibu magonjwa mbali mbali.

5

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais  Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kushoto akimpatia maelezo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama  katika halfa hiyo ya makabidhiano ya mashine kwa ajili ya kutia magonjwa mbali mbali.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

………………………………………………………………………………

VICTOR MASANGU, KISARAWE

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amekemea vitendo vya upokeaji wa rushwa  vinavyofanywa na baadhi ya wauguzi,wataalamu wa afya  na madaktari  kuwataka kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wahakikishe wanatoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa kwa kuzingatia misingi ya weledi ya kazi yao bila kuwa na ubaguzi wowote.

Jafo alitoa  kaul hiyo wakati  akizungumza na wataalamu wa afya, pamoja na wananchi wakati wa sherehe za kukabidhi mashine maalumu kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya aina mbali mbali katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambapo viongozi wa serikali madiwani pamoja na viongozi wa dini waliweza kushiriki katika zoezi hilo.

Aidha Waziri Jafo alibainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha sekta ya afya  kuanzia ngazi za maeneo ya vijijini kwa kuongeza ujenzi mpya wa zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali lengo ikiwa ni kuwaondolea adha wananchi katika suala zima la upatikanaji wa huduma ya matibabu kwa urahisi zaidi.

“Napenda kuchukua fura hii kuwambia ndugu zangu wananchi wa Kisarawe kwa kweli Rais wetu anafanya kazi kubwa sana ya kuhakikisha analeta maendeleo katika sekta mbali mbali hapa nchini na kwa sisi watu wa kisarawe tumepata bahati kubwa sana, kwa hiyo nipende kuwaambia tutaendelea kuboresha huduma ya afya katika zahanati zetu, vituo vya afya pamoja na ujenzi wa Hospitali nyingine mpya,”alisema Jafo.

Pia Jafo aliupongeza uongozi wa hospitali ya Wilaya hiyo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa kusirikiana kwa hali na mali mpaka kufanikisha kununua mashine hizo za kisasa ambazo zitaweza  kutatua changamoto za wananchi ambao hapo awali walikuwa wanapata usumbufu mkubwa kuwenda kupata vipimo katika maeneo mengine.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jonathan Budenu alisema   hospitali ya Wilaya awali  ilikuwa inakabiliwa na changamoto mbali mbali  ikiwemo ukosefu wa  vifaa tiba pamoja na upungufu wa watumishi kwa  asilimia 36 huku akibainisha  wamefanikiwa kununua mashine maalumu  za uchunguzi wa magonjwa  ambazo zimegharimu kiasi cha zaidi ya  shilingi milioni 119 fedha ambazo zimetokana na makusanyo ya ndani ya hospitali hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe  Jokate..amesema ataendelea kushirikiana bega kwa bega na viongozi wengine kwa lengo la kuweza  kuwaletea  mabadiliko chanya ya kimaendeleo wananchi wake hususana katika kuwaboresha huduma zaidi  ya afya katika zahanati,vituo vya afya na kuongeza kuwa mipango waliyonayo  ni kuifanya  hospitali  hiyo kuwa sehemu  ya mfano  katika nchi nzima.

“Jambo hili kwetu lina umuhimu mkubwa sana katika kuwaboreshea wananchi wetu huduma ya afya na kikubwa ni hapa tunamuunga Rais wetu Dr.John Pombe Magufuli katika kuhakikisha sekta ya afya inaboreshwa kwa kiwango cha hali ya juu ikiweo kununua vifaa tiba mbali mbali kama tulivyofanya katika hospitali yetu ya Wilaya kwa hiyo ni hatua kubwa”alisema Jokate.

Katika hatua nyingine Jokate amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanajiunga katika bima ya afya ambayo itaweza kuwasaidia kupata matibabu kwa urahisi na kuondokana na kero ya kusumbuka kutibiwa pindi wanapokwenda hospitalini.

Share.

About Author

Leave A Reply