Tuesday, August 20

Wanasheria zaidi ya 100 wameanza kupitia na kuchambua malalamiko mbalimbali ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam – Full Shangwe Blog

0


IMG_1871

Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Fabiola Mwingira akiwaelekeza jambo wanasheria mbalimbali wanaojitolea kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuhusu mambo ya Ardhi ikiwa ni Utekelezaji wa Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha wananchi wanatatuliwa matatizo yao kuhusu viwanja vyao,

mko1

Baadhi ya wananchi wenye matatizo mbalimbali ya ya masuala ya viwanja na wakisubiri msaada wa kisheria katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam leo.

mko2

Na John Bukuku

WANASHERIA zaidi ya 100 wameanza kupitia na kuchambua
malalamiko mbalimbali ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa
lengo la kuhakikisha yanapatiwa majibu.

Hatua hiyo inatokana na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufika
kwa Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda na kisha kutoa malalamiko
kuhusu mambo mbalimbali.

Kutokana na malalamiko hayo Makonda aliaahidi kuyashughulikia
na sasa timu hiyo ya wataalamu wa masuala ya sheria wameanza jukumu la kupitia malalamiko ya wananchi hao na kisha kutafuta ufumbuzi wake wa kisheria.

Akizungumza leo, Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Fabiola Mwingira amesema wanasheria hao wameanza kufanya uchambuzi wa malalamiko hayo na baada ya hapo wataanza
kuyasikiliza kwa kukutanisha pande zote mbili kwa maana ya mtoa malalamiko na anayelalamikiwa.

“Wanasheria hao wameanza kufanya uchambuzi wa malalamiko ya
wananchi kuanzia leo hadi Machi 9 mwaka huu na lengo
kila mwananchi aliyepeleka malalamiko yake basi yapate
ufumbuzi.

“Malalamiko wanayoyashughulikia ni yale ambayo hayako
mahakamani na yaliyo mahakamani basi yatabaki
huko huko yapatiwe ufumbuzi na tayari wamewaandikia barua wahusika,’amesema Mwingira.

Amefafanua baada ya wanashera hao kumaliza kusikiliza
malalamiko hayo, watatoa ushauri wa kisheria ambao utamuwezesha
sasa Mkuu wa Mkoa kutoa uamuzi.

Pia amesema utoaji majibu ya kero za wananchi hao awamu ya pili ,majina yatabandika kwenye geti la ofisi ya Mkuu wa Mkoa ,hivyo wananchi watatangaziwa siku na saa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.