Sunday, August 18

STATE OIL TANZANIA WAIPAISHA SERIKALI YA MAGUFULI

0


41726972_314016846090557_985786964985534152_n

Mwenendo bora wa madaraka ya serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli umepelekea kampuni ya State Oil kuweka bayana mafanikio na utofauti wa awamu ya tano.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa State Oil Tanzania Limited Anil Suchak katika mahojiano na mwandishi wa gaazeti la Jamhuri Jijini Dar es salaam ambapo alisema kwamba serikali ya awamu hii imefanya mabadiliko makubwa katika kipindi kifupi tofauti na matarajio yaa wengi pia kwenye biashara kuna maboresho makubwa katika bandari ya Dar es salaam.

Hata hivyo State Oil ni Kampuni maridhawa nchini na ni kongwe katika masuala ya mafuta, kwenye mahojiano hayo Mkurugenzi Suchak aliweka bayana mwenendo wa biashara hiyo ndani ya serikali ya awamu ya tano

“Ukweli ni lazima usemwe, hakuna kipindi kizuri cha biashara kama hiki, hapo awali tulikuwa tukikumbana na vikwazo lakini sasa hatuna tatizo ukizingatia kumekuwepo na ongezeko la uingizaji mafuta ndani ya miaka mitatu(2015-2018) kwa asilimia 11, kwa mwaka jana 2018 usafirishaji wa mafuta nje ya nchi ulikuwa asilimia 14, wakati mwaka 2015 ulikuwa ni asilimia 2 pekee, tunaamini mpaka kufikia mwaka 2020 kiwango kitaongezeka zaidi”Alisema Mkurugenzi Suchak

Aidha Suchak aligusia mageuzi mengine yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano na kutoa pongezi ambapo ni ujenzi wa ukuta, machimbo ya madini ya Tanzanite, Mradi wa kihistoria wa kufua umeme Stiegler’s Gorge, kufufuliwa kwa shirika la ndege (ATCL), Mradi mkubwa wa reli(SGR) na maboresho ya vituo vya Afya.

“Ninampongeza sana Mhe.Dk. Magufuli kwa jitihada zake na kuamua kwa dhati kutekeleza miradi hii mikubwa, kutokana na kasi hiyo nchi yetu sasa inaenda kwenye uchumi wa viwanda, na licha ya nchi yetu kuwa na vyama vingi ni jukumu la kila mtanzania kuungana ili kuisaidia serikali lango la kujenga nchi”

Ikumbukwe kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizobarikiwa kuwa na rasilimali za kipekee duniani licha la rasilimali hizo nchi imekuwa tegemezi,. Mwaka 2015 Tanzania ilifanya uchaguzi na Dokta John Pombe Magufuli akachakuliwa kuwa rais wa awamu ya tano ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali imekuwa ikitekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ambayo waau mbalimbali wameipongeza kwa mafanikio.

Share.

About Author

Leave A Reply