Saturday, August 24

KHERI JAMES AWAPA MATUMAINI MAKUBWA VYUO VIKUU.

0


DODOMA. Mwenyekiti UVCCM taifa na mjumbe wa kamati ya Chama cha Mapinduzi taifa ndugu Kheri James leo machi 24, 2018 ametoa matumaini mapya kwa vijana wa vyuo na vyuo vikuu wa Chama cha Mapinduzi leo Dodoma kipindi akifungua kikao cha wenyeviti na makatibu wa seneti mikoa wa Tanzania bara na Zanzibar.

Ndugu Kheri akiwa katika mazungumzo na viongozi wa seneti za vyuo na vyuo vikuu za mikoa (wenyeviti na makatibu) katika ukumbi wa NEC White house Mjini Dodoma amewaomba vijana wa vyuo na watu wengine kutolalamika badala yake kuwa wa kwanza kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili.

“wasomi msiwe kwenye kundi la watu wanaolalamika lazima Muwe kwenye kundi la wanaotafuta suluhisho maana Chama kinawategemea nendeni mkakisaidie,” alisema Kheri.

Kheri amewashauri na kuwataka vijana wasomi katika kadhia mbalimbali kuangalia dira ya nchi na kutoa njia za kupitia ili kuweza kufanikisha malengo ya sera za taifa katika kujiletea maendeleo nchini.

“Sisi kama viongozi wa vijana tunataka kuona idara ya vyuo vikuu ikitafsiri mwelekeo wa Serikali, muwe wakalimani wa sera za Serikali na chama chetu” alisema Kheri.

Aidha, Mwenyekiti huyo wa Umoja wa vijana UVCCM Taifa amempongeza Rais Magufuli kwa kufanya kazi kubwa kwa Nchi yetu,huku akiwataka vijana nao kufanya kazi kwa kupambana na wasomi pia kumuunga mkono Rais kwa vitendo.

“Rais Magufuli anafanya kazi kubwa kwa Nchi yetu lakini kazi anazofanya zimewapata wapinzani, sasa vijana lazima tutoke tupambane kumuunga mkono Rais wetu ” Kheri James

Hali kadhalika Ndugu Kheri James amewashauri kutokata tamaa na kuacha kulalamika na kubaki wakisubiri baraka katika serikali ya awamu ya tano bali amewataka viongozi kutengeneza mazingira ya kujitolea kwa ajili ya kuonyesha ufanisi na umahiri wa kile walichokipata vyuoni katika jamii.

“Tunataka kuona jinsi gani wasomi mnairudisha elimu mnayopata kwa jamii maana elimu ni baraka, lazima Seneti mtengeneze mazingira ya wasomi kujitolea” aliongezea Kheri.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.