Monday, August 19

ZLATAN KUPEWA NAFASI SWEDEN? – Bingwa

0


MANCHESTER, England

NYOTA wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, huenda akarejea kuvaa uzi wa timu yake ya Taifa ya Sweden.

Mpachikaji mabao huyo alishatangaza kustaafu soka la kimataifa lakini kuna uwezekano wa kuibukia Urusi zitakakofanyika fainali za Kombe la Dunia.

Ibrahimovic hajacheza tangu kuanza kwa msimu huu kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata Desemba, mwaka jana.

“Nataka kuwa na kiwango kizuri, nimekuwa nje msimu mzima kutokana na majeraha yaliyonikabili, nikiwa tayari naamini nitafanya vizuri,” alisema staa huyo mwenye umri wa miaka 36.

Kabla ya kutangaza uamuzi wake wa kuiacha, alikuwa ameichezea Sweden mechi 116 na kuifungia mabao 62.

The post ZLATAN KUPEWA NAFASI SWEDEN? appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.