Saturday, August 24

Zidane amfukuza Bale rasmi

0


MADRID, Hispania

STRAIKA Gareth Bale huenda akawa amefukuzwa rasmi katika timu ya  Real Madrid, baada ya jana kocha wake, Zinedine Zidane, kumsugulisha benchi wakati wa mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu Hispania, LaLiga ambao walifungwa mabao  2-0  wakiwa nyumbani dhidi ya  Real Betis.

Wakati wa mchezo huo ambao ulimalizika kwa mashabiki kukwaruzana na kocha na wachezaji, mbali na kutopangwa Bale hakuweza kupasha hata misuli joto kwa ajili ya kujiandaa kuingia uwanjani.

Inaelezwa kwamba, mechi hiyo ndiyo Bale angewapungia mashabiki mkono wa kwa heri wakati akiangalia ustaarabu kwa ajili ya msimu ujao.

Mfaransa huyo alitaka kuzitumia mechi 11 zilizokuwa zimebaki msimu huu tangu alipokabidhiwa mikoba ya mtangulizi wake, Santiago Solari, ili kuifanya timu ifanye vizuri lakini matokeo yake akajikuta akiboronga zaidi.

Kipigo hicho ni cha 17 kwa msimu huu kikiwa ni chini kwa vipigo  19 walivyovipata msimu wa 1984-85.

Share.

About Author

Leave A Reply