Sunday, December 16

Yanga kuwakosa Ajib na Ngasa mchezo na Biashara, Zahera ajihami

0


Lulu Ringo, Dar es salaam.

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Mkongo, Mwinyi Zahera amesema anatambua
mchezo unaoikabili timu yake  Jumapili,
Disemba 9 dhidi ya Biashara United ya mkoani Mara, ni mgumu kwakua anakutana na
timu ilioko nafasi ya mwisho katika ligi.

Zahera amesema mara nyingi mechi za timu zilizo katika nafasi za
mwishoni huwa ni ngumu kutokana na timu hizo kucheza kwa kujituma ili
kujikwamua katika nafasi zilizopo.

“Najua mchezo wetu na biashara utakuwa mgumu sana , naelewa shida
iliyopo pale tunapokutana na timu iliyo nafasi ya mwisho, huwa inajipanga
kuhakikisha inapata alama tatu ili kujikwamua huko ilipo,” amesema Zahera.

Aidha Zahera amewataka wachezaji wake kupambana kufa kupona ili
waendeleze rekodi nzuri waliyonayo ya kutopoteza mchezo wowote na kikubwa zaidi
ni kuhakikisha wanajikusanyia alama tatu.

“Wachezaji wanapaswa kujitayarisha kisaikolojia nawaomba wawe na utayari
wa kucheza mchezo huo,  nitakuwa mkali
sana kwa wachezaji wangu katika mechi hiyo, ” amesema Kocha huyo.

Zahera amesema Yanga itawakosa wachezaji wake muhimu katika mchezo huo,
Ibrahim Ajib(kadi Tatu za njano) na Mrisho ngasa (kadi nyekundu), aidha Papy
Tshishimbi na Kelvin Yondani waliokosekana katika michezo mitatu iliyopita
watakua ni sehemu ya kikosi kitakacho kutana na Biashara.

Share.

About Author

Leave A Reply