Thursday, August 22

WEMA SEPETU ACHAFUA MITANDAO – Bingwa

0


MWISHONI mwa wiki mrembo Wema Sepetu amezua gumzo katika mitandao ya kijamii, baada ya kuvuja kwa video inayomwonyesha akicheza wimbo wa rapa Zaiid (Wowowo), kwenye hafla ya kuogelea (BBQ &Pool Party), iliyofanyika Hoteli ya Gezat, Bagamoyo, juzi.

Ndani ya bwawa la kuogelea alionekana Dj wa Diamond Platnumz (Romy Jons) na Wema Sepetu ambaye alikuwa amevaa kivazi cha kuogelea, huku akionyesha umahiri wa kucheza wimbo Wowowo, kwa kutingisha sehemu ya nyuma ya mwili wake, hivyo kufanya awe gumzo katika mitandao ya kijamii.

Hafla hiyo iliambatana na sherehe ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa mwanamitindo nyota nchini, Martin Kadinda, huku mastaa kama Shilole, dada wa Diamond Esma, Aunt Ezekiel na Mose Iyobo wakihudhuria.

The post WEMA SEPETU ACHAFUA MITANDAO appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.