Wednesday, August 21

Wambura mambo bado magumu kortini

0


NA KULWA MZEE

ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura, anaendelea kusota rumande kwa zaidi ya miezi mitatu sasa na Jamhuri imedai mahakamani kuwa upelelezi haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Fatma Waziri, alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina, wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa.

Wakili Fatma alidai kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, lakini upelelezi haujamilika, hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa na kwamba upelelezi ukikamilika wataeleza.

Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Juni 4, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa anaendelea kusota gerezani, kwa sababu mashtaka yake hayana dhamana.

Wambura anakabiliwa na mashtaka 17, yakiwamo mawili ya kutakatisha Sh milioni 100.9.

Awali ilidaiwa mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka 17, yakiwamo 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, mawili ya kutakatisha fedha, moja la kughushi na moja la kuwasilisha nyaraka ya kughushi TFF.

Share.

About Author

Leave A Reply