Monday, June 17

Viongozi Simba kushuhudia Simba ikipangiwa timu Misri

0


Elizabeth Joachim, Dar es salaam

Ofisa Mtendaji Mkuu, Crescentius Magori na Mwenyekiti wa timu ya Simba, Swedi Mkwabi, wapo nchini misri kuhudhuria hafla ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika Machi 20 kwenye hotel ya Marriot iliyopo Jijini Cairo nchini humo.

Viongozi hao wa Simba wameondoka Tanzania Machi 19 kwenda nchini huko kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika.

Simba itapangwa katika droo hiyo baada ya kuvuka hatua ya robo fainali kwa kuipiga bao 2-1 timu ya AS Vita Club ya Congo, DRC.

Katika taarifa iliyotolewa na klabu ya Simba Machi 19 Jijini Dar Es Salaam imeeleza kwamba viongozi hao wameshafika nchini misri.

Simba imetinga hatua ya robo fainali pamoja na Al Ahly ya misri iliyoongoza kundi D. Timu nyingine zilizotinga hatua hiyo ni
pamoja na Mabingwa watetezi wa kombe hilo Esperence ya Tunisia, Mamelodi SunDowns ya Afrika Kusini, Wydad Casablanca ya Morocco, Haroya AC ya Guinea, TP Mazembe ya Congo na CS Constantine kutoka Algeria.
Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya Tanzania kufika robo fainali katika kinyang’anyiro hicho cha kuwania kombe la Mabingwa Afrika baada ya miongo minne. Mwaka 1974 ilikuwa ndio mara ya mwisho kwa Simba kufika hatua ya robo fainali ya kombe hilo.

Share.

About Author

Leave A Reply