Friday, May 24

Vanessa Mdee, Lil Ommy wapamba jarida kubwa Nigeria

0


NA CHRISTOPHER MSEKENA

STAA
wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee na mtangazaji nyota Bongo, Omary Tambwe ‘Lil
Ommy’, wamepamba toleo la 23 la jarida kubwa la Tush Magazine, linaloangazia
vijana wenye mafanikio kwenye sekta za burudani Afrika.

Vanessa
alipamba ukurasa wa mbele wa Tush Magazine huku sababu kubwa ikiwa ni historia
yake ya muziki kutoka alivyoanza mpaka alivyopata mafanikio, huku Lil Ommy
(King Of Interviews, The MVP) naye akipamba ukurasa wa ndani kwa makala
inayoelezea mafanikio aliyonayo sasa kwenye utangazaji wa vipindi vya burudani.

Jarida
hilo lenye mrengo wa vijana, limesheheni habari, mahojiano na makala za mastaa
mbalimbali katika tasnia za muziki, mitindo, filamu, teknolojia, matamasha, mahusiano
na biashara.

Share.

About Author

Leave A Reply