Tuesday, August 20

‘TRA’ wamshukia Diego Costa 

0


MADRID, Hispania

MAMLAKA zinazoshughulika
na masuala ya kodi nchini Hispania, zimemtia hatiani straika wa Atletico
Madrid, Diego Costa, kwa madai ya ukwepaji kodi.

Imedaiwa
kuwa mpachika mabao huyo wa Atletico, alilipwa kiasi cha euro milioni moja kwa
njia isiyofaa mwaka 2014 aliposajiliwa na klabu ya Chelsea.

Kwa mujibu
wa ripoti ya kodi, malipo hayo yalifanyika tofauti na kiasi cha awali cha Euro
milioni 2.3.

Mamlaka hayo
yamemtuhumu Costa kwa kitendo cha kuficha malipo yake kupitia mikataba ya udhamini
kutoka Kampuni ya Adidas, siku chache kabla ya kutua Chelsea.

Aidha, madai
hayo yameripotiwa kumweka Costa kwenye wakati mgumu na huenda akaikacha Atletico
na kuhamia kwingineko ndani ya Bara la Ulaya.

Share.

About Author

Leave A Reply