Saturday, August 17

TID: Sina tatizo na Lulu Diva, nipo tayari kumpa mtoto

0


NA MWANDISHI WETU

MKALI wa Bongo Fleva, Khalid
Mohamed ‘TID’, amesema hana tatizo na msanii Lulu Diva, baada ya kukaririwa
akimtuhumu mrembo huyo kuwa amezaa na anamficha mtoto wake.

Akizungumzia ishu hiyo jana
kwenye kipindi cha XXL ya Clouds Fm, TID, alisema kuna mwandishi alimuuliza
nini maoni yake kuhusu Lulu Diva ambaye ana mtoto na anamficha.

 “Mimi sina tatizo na Lulu Diva, inabidi watu wajiulize hayo maneno yalianzia wapi, mimi niliambiwa ana mtoto na mwandishi aliniuliza maoni yangu kuhusu hilo, kama Lulu anapenda mtoto na hana mtoto mimi nipo hapa nitampatia mtoto nina mbegu za kutosha,” alisema TID, anayefanya vyema na wimbo Jigy Jigy.

Idea atoa siri ya kimya chake, aachia Wathamani

NA MWANDISHI WETU

BAADA ya mashabiki kumtaka msanii wa Bongo Fleva anayeliwakilisha vyema Jiji la Mwanza, Iddi Mussa ‘Idea Tz, aachie wimbo mpya, mwimbaji huyo ametoa sababu za kimya chake.

Idea Tz, aliyewahi
kufanya vizuri na wimbo Sichoki, ameliambia Papaso la Burudani kuwa alikaa
kimya ili kuusoma muziki na sasa amerudi upya na video ya wimbo wake Wathamani.

 “Huu muziki ni biashara, hivyo lazima ufanye
mahesabu vizuri, ndiyo maana nilikuwa kimya, nashukuru mashabiki wamekuwa
wakinisubiri na sasa nimeachia video mpya ambayo inafanya vizuri toka itoke,”
alisema Idea.

Mwakangale atupia dansi kwenye Injili

NA CHRISTOPHER
MSEKENA

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili, Joseph Mwakangale, amesema sababu za kuchanganya vionjo vya dansi kwenye wimbo wake mpya, Maneno Yao ni kutaka kumtukuza Mungu tofauti na ilivyozoeleka.

Akizungumza na
Papaso la Burudani, Mwakangale alisema imezoeleka kuwa injili ni muziki wa
taratibu, lakini yeye ameamua kuwa tofauti ili kuleta ladha mpya.

“Sijafanya muziki wa dansi, ila nimetumia vionjo na mirindimo ya dansi katika kumtukuza Mungu kwa njia tofauti na ile iliyozoeleka,” alisema Mwakangale.

Pierre anogesha Kesho ya Dragon

N JEREMIA ERNEST

MNYWAJI wa pombe maarufu zaidi mtandaoni kwa sasa, Peter Mollel ‘Pierre’, ameendelea kupasua anga la mafanikio mara baada ya msanii wa Bongo Fleva, Juma Ramadhan ‘Dragon’, kumshirikisha katika wimbo Kesho.

Akizungumza na Papaso la
Burudani, Dragon alisema anashukuru wimbo huo umepata mapokezi makubwa, tofauti
na alivyotarajia kutokana na Pierre kuonyesha uwezo wa hali ya juu.

“Nashukuru wadau kwa kuipokea vyema nyimbo yangu imepata mapokezi makubwa kuliko matarajio yangu, Pierre ana uwezo katika sanaa,” alisema Dragon.

Aysher Vuvuzela kutambulisha ujio mpya Mei 3

NA JEREMIA ERNEST

MWANAMUZIKI nyota wa taarabu nchini, Aysher Vuvuzela, ameweka wazi kuwa ujio wa bendi yake mpya utatambulishwa Mei 3 mwaka huu, katika ukumbi wa New Friends Corner, Manzese, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Papaso la
Burudani jana, Vuvuzela alisema bendi hiyo, ambayo ametumia mwaka mmoja
kuitengeneza, itakuwa inapiga muziki wa taarabu asili pamoja taradansi kwenye
kumbi mbalimbali za burudani.

“Bendi itakuwa na wanamuziki
watano na nitawatambulisha siku ya uzinduzi pamoja na nyimbo mpya, ukiwamo ule
wa Mjini Nyota, ambao ameimba mwenyewe, tutasindikizwa na msanii wa Singeli,
Msaga Sumu, Matarumbeta kwa kiingilio cha shilingi 5,000,” alisema Vuvuzela.

Share.

About Author

Leave A Reply