Sunday, August 25

TBF wahaha kusaka wadhamini

0


NA GLORY MLAY

SHIRIKISHO la
Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), linaendelea kusaka wadhamini ili kufanikisha
maandalizi ya michuano ya FIBA ya Kanda ya Tano kwa timu za vijana chini ya
umri wa miaka 16, itakayofanyika Juni, mwaka huu.

 Akizungumza na BINGWA jana, Rais wa TBF,
Phares Magesa, alisema Tanzania wanatarajiwa 
kuwa wenyeji wa michuano hiyo.

Magesa alisema wanahitaji
udhamini na msaada wa wadau ili kufanikisha maandalizi ya michuano hiyo.

Pia alisema wanahitaji
nguvu ya wadau ili waweze kufanyia marekebisho ya Uwanja wa Ndani wa Taifa
kabla ya michuano hiyo.

Magesa alisema
pamoja na maandalizi mengine, lakini timu zinatakiwa kuanza maandalizi mapema
ili ziweza kufanya vizuri.

“Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba wadau mbalimbali wenye mapenzi na mchezo huu kujitokeza na kuzipa nguvu timu hizi ili ziweze kutuwakilisha vyema,” alisema Magesa. Magesa alisema vijana hao wanatarajia kuingia kambini Mei mwaka huu,  Monduli mkoani Arusha .

Share.

About Author

Leave A Reply