Sunday, August 18

Tanzania, Zimbabwe kuchuana kriketi Mei 6

0


NA GLORY MLAY

TIMU ya taifa ya kriketi ya wasichana  inatarajia kushuka  uwanjani Jumatatu ijayo kucheza na Zimbabwe
katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, utakaochezwa kwenye Uwanja wa
Harare nchini humo.

Katika michuano hiyo, Tanzania imepangwa Kundi A pamoja na Nigeria,
Msumbiji, Rwanda na Zimbabwe na Kundi B linaundwa na Uganda, Kenya, Namibia na
Sierra Lione.

Akizungumza na BINGWA jana, Abdallah Khamis alisema pamoja
na kupangiwa kundi gumu, anaamini watafanya vizuri kutokana na maandalizi ya
muda mrefu waliofanya wachezaji wake.

Khamis alisema wamejipanga kiushindani kwani wanajua wanakwenda
kukutana na wachezaji wazoefu katika michuano hiyo.

Alisema wachezaji wake wapo fiti kwa ajili ya michuano hiyo.

Share.

About Author

Leave A Reply