Sunday, August 18

Staa Liver achekelea wanavyoibana Man City

0


LONDON, England

STAA James Milner amesema kwamba anafurahi kuona
timu yao ya Liverpool ikiendelea kuibana Manchester City  katika vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu
England.

 Vijana hao wa
Jurgen Klopp juzi walifanikiwa kurejea tena kwenye msimamo wa Ligi Kuu England,
baada ya kuichapa mabao 2-0 timu ya Cardiff City, yaliyofungwa na mastaa
wao,  Georginio Wijnaldum na James Milner
kipindi cha pili cha mtanange huo.

 Matokeo hayo
yameifanya Liverpool kuwa mbele kwa pointi mbili dhidi ya wapinzani wao hao Man
City ambao bado wana mechi moja kibindoni.

Vijana hao wa Pep Guardiola wanaweza kuendelea kukaa
kileleni endapo kesho wataondoka na ushindi dhidi ya Manchester United, wakiwa
ugenini Old Trafford na Milner anakiri akisema kwamba, walau Liverpool imeweka
ugumu kwa mabingwa hao watetezi kutetea kirahisi taji lao.

“Tutaendelea kuwapa presha kwa kushinda mechi
zetu zote,” kiungo huyo wa zamani wa Man City aliiambia Sky Sports.

“Itawawia vigumu kwani kama tungeteleza
ingekuwa rahisi kwao,” aliongeza nyota huyo.

Share.

About Author

Leave A Reply