Thursday, August 22

SOURFA kuanzisha soka la vijana, wanawake Unguja

0


NA IBRAHIM MAKAME, ZANZIBAR

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Soka Mkoa wa Kusini Unguja (SOURFA),
imekutana kwa mara ya kwanza jana, tangu kuchaguliwa kwake Aprili 12, mwaka huu
na kuazimia kuanzisha soka la vijana na wanawake.

Kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti wake, Shauri Hassan Juku,
kilifanyika jana asubuhi kwenye Ukumbi wa Shule ya Kibele, visiwani hapa.

Akizungumza na BINGWA jana, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Abubakar
Khatib Kisandu, alisema lengo la kikao hicho lilikuwa ni kukabidhiana majukumu
ya kazi.

Kisandu alisema kikao hicho pia kilijadili masuala mbalimbali, ikiwamo
mipango  ya maendeleo ya chama hicho.

Alisema waliweza kujadili namna ya kuendesha michuano ya wilaya na mkoa.

Kisandu alisema kikao hicho kiliunda kamati mbalimbali za michuano za mkoa
huo.

Alisema wajumbe wa kikao hicho walipitisha malengo makuu, yakiwamo
kuanzisha soka la vijana na wanawake ambalo limekuwa ni changamoto kubwa kwa Mkoa
wa Kusini Unguja, ili kuweka misingi imara ya soka.

‘’Tunaomba ushirikiano na wadau wa mpira wa Mkoa wa Kusini Unguja kwa
lengo la kuona tunafanya bidii kubwa ili kuwa na soka la vijana na wanawake
kuanzia ngazi za vijana,’’ alisema Kisandu.

Share.

About Author

Leave A Reply