Sunday, August 18

Souness aeleza ukweli wa Man Utd ya miaka ijayo

0


MANCHESTER, England

MKONGWE wa
zamani wa timu ya Liverpool, Graeme Souness, anaamini kuwa itapita misimu
kadhaa ya usajili ambayo klabu ya Manchester United itatumia fedha nyingi mno
kutengeneza timu ya kutwaa mataji.

Kauli hiyo
ya Souness imekuja baada ya kushuhudia mashetani wekundu hao waking’olewa na Barcelona
kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mapema wiki hii kwa jumla ya mabao 4-0.

Kwa mujibu
wa mchambuzi huyo wa soka, wachezaji wengi wanaoitumikia United ni aidha wana
uwezo usiojitosheleza au wasio na hadhi ya kuendelea kuwepo Old Trafford.

Kama hiyo
haitoshi, Souness alidai kuwa hajashawishika na Ole Gunnar Solskjaer kuwa ndiye
kocha atakayefaa kudumu Man Utd kwa muda mrefu.

“Solskjaer
na Man Utd kwa ujumla watahitaji muda mrefu wa kujisuka upya. Hakuna njia ya
mkato itakayowapa mafanikio. Nazungumza kama mtu wa soka, kibarua alichokipata
Ole ni kizito,” alisema Souness.

“Man Utd
itahitaji wachezaji wengi bora zaidi ya vijana wao kutoka akademi, United
wanahitaji nyota katika soko la usajili. Si kwa mwaka mmoja, bali ni miaka
kadhaa inayokuja.

“Makocha
waliopita hawakufanya sajili za kueleweka sana. Ili Man Utd wanase mafanikio
wakiwa na Solskjaer, wanatakiwa kubadilisha namna wanavyofanya usajili.

“Wachezaji
waliocheza dhidi ya Barcelona hawana hadhi ya kuendelea kuwepo pale kwa miaka
minne hadi mitano kuanzia sasa. Tofauti na hapo, itabidi tusubiri kama
watapandisha viwango vyao na kuwa wachezaji muhimu zaidi kwa United,” alisema.

Aidha, Souness
aliongeza kuwa, kutokana na presha kubwa ya United kurudi kwenye mstari na
kushinda mataji kama zamani, huenda wakaingia kwenye mtego wa kutumia mamilioni
ya pauni katika soko la usajili, japo wanaweza pia wasifanye hivyo.

Share.

About Author

Leave A Reply