Thursday, August 22

Solskjaer alianzisha Old Trafford

0


MANCHESTER, England

OLE
Gunnar Solskjaer amewajia juu nyota wake, akisema hawakujitoa vya kutosha dhidi
ya Barcelona na ndiyo maana walitolewa Ligi ya Mabingwa kwa kichapo cha jumla
ya mabao 4-0.

Katika
mchezo wa kwanza uliochezwa Old Trafford, Mashetani Wekundu walilala bao 1-0,
kabla ya kichapo kizito cha mabao 3-0 pale Nou Camp wiki moja baadaye.

Mtandao
wa SunSport ulikuwa wa kwanza kuripoti kuwa Solskjaer alikuwa mbogo mbele ya
wachezaji wake baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo wa Hispania, akiwaambia
hawakujitoa kwa asilimia 100 kukabiliana na Lionel Messi na wenzake.

Kilichomvuruga
zaidi kocha huyo raia wa Norway ambaye aliwahi kuwa mshambuliaji tishio Man
United, hicho kilikuwa kipigo cha tano katika mechi saba za hivi karibuni.

Share.

About Author

Leave A Reply