Thursday, August 22

SNURA AWANG’ATA SIKIO MASTAA SIMBA – Bingwa

0


NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya Simba kuondolewa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Staa wa Bongo Fleva, Snura Mushi,  amewang’ata sikio wachezaji wa timu hiyo, akiwataka kuelekeza nguvu kwenye ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba ilitolewa na Al Masry  ya Misri,  licha ya kutofungana katika mchezo wa marudiano uliochezwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Port Said.

Hata hivyo, Al Masry  walisonga mbele baada ya kupata sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Nimesikitika  Simba kushindwa kusonga mbele,  lakini nashukuru vijana walipigana kiume,  kazi iliyobaki ni kupigania ubingwa wa ligi,”  alisema Snura.

Snura ambaye ni shabiki mkubwa  wa Simba, alisema wachezaji wa timu hiyo wanatakiwa kuelekeza akili yao Ligi Kuu ili waweze kutimiza malengo yao.

Alisema kutokana na kiwango cha wachezaji wa Simba  anaimani  wataendelea kufanya vizuri Ligi Kuu na baadaye kuchukua ubingwa  ili msimu ujao waweze kushiriki mashindano ya kimataifa.

The post SNURA AWANG’ATA SIKIO MASTAA SIMBA appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.