Monday, July 22

Simba tupo nyuma yenu

0


WAWAKILISHI pekee wa Tanzania kwenye michuano ya
kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba, wanatarajiwa kucheza na timu ya JS
Saoura ya Algeria katika mchezo utakaochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.

Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa Kundi D linaloundwa
na timu za Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),
JS Saoura na Simba.

Mchezo
wa
leo ni
muhimu kwa Simba kupata ushindi ambao utaongeza morali ya wachezaji kushinda ule
utakaofuata.

Lakini ushindi kwa Simba utatoa mwelekeo wa timu
hiyo kufanya vizuri katika kundi lao hilo.

BINGWA tunasema Simba wana uwezo wa kupata matokeo
mazuri wakiwa nyumbani kwa kujipanga vizuri uwanjani na kuhakikisha pointi tatu
zinapatikana.

 Tunaamini
Simba wakianza kwa ushindi watakuwa wamejiweka katika mazingira bora ya kutinga
hatua ya robo fainali.

Tunasema kwamba, uwezo walioonyesha wachezaji wa Simba
katika hatua ya awali ya ligi hiyo, wanatuaminisha wataweza kuendelea kuwapa
furaha mashabiki wao.

 Tunaamini
kwamba, kama Simba waliweza kuvuka makundi kwa kushinda michezo tatu
iliyochezwa nyumbani na ugenini, hawatashindwa kuendeleza moto wao katika
mchezo wa leo dhidi ya wapinzani wao.

Mwaka jana, Simba walianzia nyumbani kwa kuwafunga
mabao 4-1 Mbabane Swallows ya Swaziland, baadaye kuwatoa kwa jumla ya mabao
8-1.

Katika mchezo wa marudiano, Simba walifanikiwa kuwafunga
mabao 4-0 Mbabane Swallows uliochezwa ugenini, kabla ya kufungwa mabao 2-1
Nkana ya Zambia katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza, kisha Simba
kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

BINGWA tunaamini Simba wanaweza kuendeleza wimbi la
ushindi leo iwapo wachezaji wa timu hiyo watacheza kufa au kupona uwanjani.

Lakini tunatoa tahadhari kwa wachezaji wa Simba kutowadharau
JS Saoura kwa kuwa wanakuja nchini wakiwa wamejipanga kwa lengo la kupata
ushindi.

BINGWA tukiwa wadau wa kwanza wa michezo hususan
soka, tunasema tupo nyuma ya Simba kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo
wa leo dhidi ya wapinzani wao, JS Saoura.

Share.

About Author

Leave A Reply