Saturday, August 24

Shindano la keki lawavutia Shilole, Esha Buheti

0


NA KYALAA SEHEYE

WAREMBO wanaofanya vizuri kwenye muziki na filamu ambao pia ni wajasiriamali wa chakula, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Esha Buheti, wamevutiwa na shindano la keki linaloandaliwa na Zena Sharif ‘Anazelitta’.

Wawili hao, wamesema kwa kuwa nao ni wajasiriamali basi haina ubaya kuiga mazuri yanayofanywa na mjasiriamali mwenzao ili kuzidi kuinua wengine na wao pia kujitangaza.

“Mimi huwa sijali mtu akinisema kwa kuiga mazuri, kama yeye amefanya mashindano ya kupika keki basi mimi kwa kuwa mama lishe naweza kuandaa hata mashindano yanayoendana na biashara yangu, naimani nitaweza kunyanyua Mtanzania mmoja ambaye    ataweza kujitegemea,” alisema Shilole.

Hali kadhalika, Esha aliongeza kuwa yuko pamoja na Shilole na wana imani watakaa chini na kulifanyia kazi wazo hilo ili kuweza kuhakikisha wanarudisha fadhila kwa mashabiki wao.

Share.

About Author

Leave A Reply