Wednesday, August 21

Shaqiri basi tena Liverpool

0


MERSEYSIDE, England

LIVERPOOL wanaweza kumuuza staa wao wa kimataifa wa Uswis, Xherdan Shaqiri, katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi endapo watapewa ofa ya maana.

Hadi kumalizika kwa msimu huu, nyota huyo alikuwa ameifungia Liverpool mabao sita, huku akitoa ‘asisti’ tano katika mechi 30.

Imeripotiwa kuwa Shaqiri (27) ataondoka licha ya kwamba amebakiza miaka minne katia mkataba wake wa sasa.

Share.

About Author

Leave A Reply