Friday, May 24

Rayvanny agawa mafuta kwa bodaboda

0


NA BRIGHER MASAKI

MKALI
wa Bongo Fleva, Raymaond Mwakyusa ‘Rayvanny’, ameendelea kujiweka karibu na
mashabiki zake mara baada ya jana kugawa mafuta kwa madereva bodaboda na bajaji
katika sheli ya State Oil, iliyopo Sinza Afrikasana, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza
na mashabiki zake katika tukio hilo lililowavuta watu wengi, Rayvanny alisema
ameamua kufanya hivyo kwa sababu anaamini waendesha bodaboda ni mashabiki zake
wakubwa na wamekuwa wakimpa sapoti kwenye muziki wake.

“Kama
unavyoona hapa bajaji na bodaboda zote zina picha yangu, huu ni upendo mkubwa
sana, ndiyo maana nikaona kwa kidogo nilichojaliwa nigawe mafuta na niweke
saini yangu kama shukrani,” alisema memba huyo wa WCB.

Share.

About Author

Leave A Reply