Friday, March 22

Ratiba Ligi Kuu yapanguliwa tena

0

Na Mwandishi Wetu

Bodi ya Ligi ya Tanzania Bara (TPLB) imefanya mabadiliko ya michezo minne ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Mchezo kati ya Yanga Sc dhidi ya Biashara United umesogezwa mbele kwa masaa matatu badala ya kupigwa kesho Jumapili saa 10:00 jioni sasa mchezo huo utapigwa saa 1:00 usiku siku hiyo hiyo

Mchezo wa kiporo kati ya Simba dhidi ya KMC sasa utapigwa Jumatano ya Disemba 19 katika uwanja wa Taifa Dar majira ya saa 12:00 Jioni

Pia mchezo namba 170 kati ya KMC na TZ Prisons uliotakiwa kupigwa Disemba 17 umerudishwa nyuma na sasa utachezwa Disemba 15 katika dimba la Uhuru

Vilevile mchezo kati ya Lipuli Fc dhidi ya Ruvu Shooting uliotakiwa kupigwa jana Disemba 7 sasa utapigwa keshokutwa Disemba 10 kati uwanja wa Samora Iringa.Share.

About Author

Leave A Reply