Friday, August 23

RAPA NIGERIA ACHOMOKA GEREZANI MAREKANI – Bingwa

0


LOS ANGELES, Marekani

STAA wa hip hop raia wa Nigeria, Sauce Kid, ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo chake cha miaka miwili gerezani nchini Marekani.

Mkali huyo alipewa adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika wizi wa fedha benki kwa kutumia namba za siri feki.

Kwa kipindi chote hicho kabla ya kukamatwa, jamaa alikuwa ameshajiingizia Dola 15,388.

Kid alianza kujizolea umaarufu katika soko la muziki la Nigeria mwaka 2005 baada ya kutoka na ngoma yake kali ya ‘Omoge’.

Mwaka uliofuata, akaachia ‘mixtape’ aliyoiita ‘Best of Both Worlds: Money Long The Mixtape’, ambayo ndiyo iliyomtangaza zaidi kwa mashabiki wa tasnia ya burudani.

The post RAPA NIGERIA ACHOMOKA GEREZANI MAREKANI appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.