Thursday, August 22

PSG NOMA, WAMALIZANA NA FABIHNO – Bingwa

0


PARIS, Ufaransa

MTANGAZAJI wa kituo cha televisheni cha Canal +, Olivier Tallaron, amefichua kuwa kiungo wa Monaco raia wa Brazil, Fabinho, anakaribia kutua PSG.

Fabinho mwenye umri wa miaka 24, alikuwa na mchango mkubwa kwa Monaco msimu uliopita, akiipa taji la Ligi Kuu ‘Ligue 1’.

Timu hiyo yenye maskani yake jijini Paris, iliishia robo fainali baada ya kung’olewa na Real Madrid kwa kichapo cha jumla ya mabao 5-2 katika mechi mbili.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, dili hilo linatakiwa likamilike mapema, ikiwezekana kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia.

PSG wanataka kukisuka upya kikosi chao ifikapo Juni, mwaka huu, baada ya kuvurunda katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

The post PSG NOMA, WAMALIZANA NA FABIHNO appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.