Sunday, August 25

Pochettino: Wachezaji wangu ni mashujaa

0


LONDON, England

KOCHA wa Tottenham,
Mauricio Pochettino, amesema wachezaji wake ni mashujaa baada ya kuibuka na
ushindi wa mabao ya ugenini dhidi ya Man City na kufanikiwa kutinga nusu
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Spurs
iliivaa Man City usiku wa kuamkia jana, lakini licha ya kutandikwa mabao 4-3,
walifanikiwa kuing’oa City kwenye Ligi ya Mabingwa kwa sheria ya bao la ugenini
kutokana na kushinda mechi ya nyumbani bao 1-0.

Kichapo
hicho kilikamilisha misimu mitatu mfululizo ambayo imeshuhudiwa Man City ya Pep
Guardiola ikishindwa kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Nina
furaha. Najivunia kupita kiasi kutimiza ndoto hii ya kucheza nusu fainali.
Wachezaji wangu wameonesha ushujaa,” alisema Pochettino.

“Mechi mbili
dhidi ya Man City zilikuwa ni kama fainali, lakini tumeonesha upinzani na
kushinda. Tumedhihirisha kila kitu kinawezekana katika mchezo wa soka,”
alisema.

Share.

About Author

Leave A Reply