Monday, August 19

Pochettino: Mlituchukulia poa Uefa

0


LONDON, England

MKUU
wa benchi la ufundi la Tottenham, Mauricio Pochettino, amesema hakuna aliyekuwa
akiipa timu yake nafasi lilipokuja suala la timu zitakazofika nusu fainali ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ikiwa
imepangwa kundi lililokuwa na PSV, Inter na Barcelona, Tottenham waliingia
hatua ya mtoano wakishika nafasi ya pili, ikichangiwa na sare yao dhidi ya
Barca katika mchezo wa mwisho.

“…
Mwanzoni mwa msimu hakuna aliyeamini tungekuwa hapa,” alisema Muargentina
huyo kuwaambia waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya
Manchester City, ambao ni wa Ligi Kuu.

Pochettino
anakwenda Etihad huku kukiwa na shaka ya kumtumia Moussa Sissoko aliyeumia
katika mtanange wao dhidi ya Man City.

Share.

About Author

Leave A Reply