Sunday, August 25

PISHA NJIA… Zidane afichua jukumu la kwanza alilopewa Madrid, Barca hofu tupu

0


MADRID, Hispania

KOCHA wa timu ya Real Madrid, Zinedine Zidane,
ameweka wazi jukumu kubwa alilopewa kuwa ni kuhakikisha wananyakua taji la La Liga
msimu ujao ambalo limeshikiliwa na Barcelona kwa miaka mingi sasa.

Barca ambao usiku wa kuamkia jana waliichapa Alaves mabao
2-0, walikuwa wanasubiri kutangazwa mabingwa iwapo Valencia ingeibuka na
ushindi dhidi ya Atletico Madrid, usiku wa kuamkia leo.

Kwa muda mrefu Barca ilishatabiriwa ubingwa wa
Hispania msimu huu, wakiizidi Madrid kwa tofauti ya pointi 16, huku wapinzani
wao hao wakiwa na msimu mbovu kuwahi kutokea katika historia yao.

Hata hivyo, baada ya kumalizika kwa msimu huu, Los
Blancos hao wanatarajiwa kufungua begi la fedha na kusajili wachezaji bora
duniani ili kuhakikisha wanaipiku Barca kwenye La Liga.

“Mwakani tutakuja na nguvu mpya ili tuanze kulisaka
taji la La Liga. Tutahakikisha tunaanza ligi katika mwenendo unaoeleweka. Hilo
ndilo jambo muhimu,” alisema Zidane jana kabla ya mchezo wao dhidi ya Getafe
utakaochezwa leo.

“Ni lazima tujitume kuanzia mechi za kujipima ubavu,
la sivyo hali itakuwa mbaya kwa mara nyingine tena. Kitu cha kwanza msimu ujao
ni kushinda taji la La Liga.

“Kwa sasa tuipe heshima na pongezi Barca, wamefanya
vizuri mno lakini kwenye historia ni Real Madrid ambayo ina mataji mengi ya La
Liga, 33. Barca wanayo mangapi?

“Wanafanya vizuri katika nyakati za hivi karibuni,
hivyo jukumu letu ni kubadilisha hali hiyo, kwangu mimi muhimu ni La Liga kwa
sababu ina mechi nyingi, tofauti na Ligi ya Mabingwa Ulaya,” alisema Zidane.

Share.

About Author

Leave A Reply