Sunday, August 18

NIYONZIMA, MBONDE WAKABIDHIWA KWA PIERRE – Bingwa

0


NA MWAMVITA MTANDA

KOCHA wa viungo wa Simba, Aymen Hbibi, amesema kiungo mchezeshaji wa timu hiyo, Haruna Niyonzima na beki wa kati, Salim Mbonde, kwa sasa wapo fiti kucheza baada ya kupona majeraha.

kizungumza na BINGWA juzi, Hbibi alisema wawili hao wanaendelea vizuri, baada ya kujiunga na wenzao katika mazoezi ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hbibi alisema wachezaji hao wanaweza kucheza michezo ijayo iwapo kocha mkuu wa timu hiyo, Lechantre Pierre, ataamua kuwapanga katika kikosi chake.

“Kwa sasa wanafanya mazoezi maalumu, lakini baada ya mechi dhidi ya Njombe Mji watakuwa fiti zaidi,” alisema Hbibi.

Simba wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa baada ya kufikisha pointi 46 sawa na Yanga.

The post NIYONZIMA, MBONDE WAKABIDHIWA KWA PIERRE appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.