Monday, August 19

NI VITA – Bingwa

0


 * Ronaldo amtangazia kiama Messi Pichichi

MADRID,Hispania

STRAIKA   wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amemtangazia  vita kali mwenzake wa Barcelona, Lionel Messi, baada ya kubeti na  wenzake  akisema kwamba ni lazima atahakikisha anampuku katika mbio za kuwania kiatu cha mfungaji bora La Liga maarufu kama Pichichi.

Mabao manne aliyoyafunga juzi Ronaldo yamemfanya kubaiza matatu ili amfikie Muargentina huyo kwenye orodha ya wafungaji bora jambo ambalo linamfanya awe karibu kumpiku mpinzani wake huyo kutoka  Camp Nou.

“Hat-trick’ ambayo ilikuwa  ni  35 akiwa na  Real Madrid katika michuano hiyo ya  LaLiga ma ilimfanya kumpiku nyota mwingine wa Barca Luis Suarez baada ya kufikiasha mabao 22  jambo ambalo linampa jeuri ya kutangaza vita hiyo.

Kwa mujibu wa mtanzaji wa Kituo cha Redio MARCA ambaye anarusha kipindi cha  El Transistor,  Jose Ramon de la Morena, Ronaldo alitangaza kuanza kampeini hiyo mbele ya wenzake ili aweze kufunguka baada ya kuaanza msimu huu vibaya.

Mpaka sasa  Messi  ndiye yupo kileleni mwa msimamo wa ligi, akiwa na mabao  25 ambayo ameyafunga tangu msimu huu uanze lakini idadi kubwa ya mabao ya Ronaldo yanaonekana kupatikana tangu mwaka huu uanze.

Kauli hiyo ya sasa pia imekuja baada ya Novemba mwaka jana kuwaambia pia wachezaji wenzake kwamba ni lazima atafunga mabao   mengi zaidi kuliko ya Messi ili aweze kutwaa tuzo hiyo ya  Pichichi.

Wakati akitangaza vita hiyo staa huyo alikuwa nyumba  kwa mabao 11 jambo ambalo liliwashangaza wengi kutokana na kauli yake hiyo.

Katika mchezo huo wa juzi dhidi ya Girona, bao la kwanza la staa huyo lilipatikana dakika ya  11 kwa guu lake la kushoto akimalizia mpira aliotengewa na Toni Kroos, lakini  Girona  wakasawazisha muda mfupi kupitia kwa nyota wao, Cristhian Stuani kwa mpira wa wa adhabu.

Ronaldo aliongeza la pili mapema kipindi cha pili  na kisha akatengeneza la tatu lililowekwa kimiani na staa mwenzake, Lucas Vazquez nakisha akaongeza la nne kabla ya wapinzani wao kupata la pili kupitiua tena kwa nyota wao  Stuani  likiwa ni la tisa kwake msimu huu kwenyer michuano hiyo ya  LaLiga.

Staa aliyetokea benchi,  Gareth Bale aliingia kwenye orodha ya wafungaji wa siku zikiwa zimebaki dakika nne kabla ya mpira kumalizika  na kisha  Ronaldo  akamaliza biashara katika muda wa nyongeza.

Hii ni  mara ya    50  kwa  Ronaldo kufunga mabao  zaidi ya matatu katika mashindano yote tangu alipoanza kusakata soka.

The post NI VITA appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.