Thursday, August 22

Ngassa afunguka usajili Yanga

0


HUSSEIN OMAR

SIKU chache baada ya Yanga kufanya usajili  wa wachezaji wapya, winga wa kikosi hicho, Mrisho
Ngassa, amefunguka na kusema anaiona 
timu mpya msimu ujao.

Hadi sasa Yanga imesajili wanne, straika Issa
Bagirimana, winga Patrick Sibomana,  beki
wa kati Lamine Moro, kiungo Abdulazizi Makame Hassan na kumwongezea mkataba Papy
Kabamba Tshishimbi.

Akizungumza na BINGWA jana, Ngassa alisema usajili
uliofanywa ameanza kupata picha ya kikosi cha msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania
Bara.

“Binafsi nimefurahishwa na usajili unaoendelea, ili
mchezaji ufanye vizuri lazima nyuma yako wawepo wachezaji wengine bora, nina
imani na usajili huu kuwa ni wachezaji wazuri,” alisema Ngassa.

Ngassa bado ana msimu mzima umebaki kuendelea
kuitumikia Yanga, hivyo atakuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha timu hiyo
kwa msimu ujao.

“Nimetulia nafuatilia usajili, tutatisha msimu
ujao, niwaambie wapenzi na mashabiki wa Yanga watulie tutapata timu nzuri baada
ya kupata uongozi mpya,’’ alisema Ngassa.

Share.

About Author

Leave A Reply