Wednesday, July 17

Neymar anapatikana kwa bei chee tu!

0


PARIS, Ufaransa

IMERIPOTIWA PSG
imeshusha bei ya kuuzwa kwa staa wao Neymar, inayodaiwa kupungua na kufikia
pauni milioni 63 (sh bil.144) kumuachia mchezaji huyo.

Awali, bei ya Neymar
imetajwa kuwa thamani ya pauni milioni 135 (sh bil. 309), na sasa wapo tayari
kumpoteza kwa pesa hiyo ya sasa ambayo imetajwa.

Imeaminika nyota huyo ameishikiza PSG, kumwachia
kurejea katika klabu yake ya zamani, ya Barcelona msimu ujao.

Mkurugenzi wa michezo wa PSG, Leornado
aliliambia gazeti la  Le
Parisien
, wapo tayari kumuachia Neymar, endapo ofa nzuri italetwa
mezani.

Naye baba wa mchezaji huyo amethitibisha
sababu ya kuchelewa, kuripoti mazoezini kwa mchezaji huyo, ni  kutokana 
na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Share.

About Author

Leave A Reply