Monday, August 26

Ndayiragije kutambulishwa Azam FC fainali ya ASFC

0


NA ZAINAB IDDY

UONGOZI wa Azam FC umepanga kumtangaza kocha wao mpya, Etienne Ndayiragije, wakati timu yao itakapokuwa ikicheza fainali ya Azam Sports Federation Cup ‘ASFC’, Juni 1, mwaka huu.

Azam FC itakuwa na kibarua kigumu cha kuwania taji hilo la ASFC dhidi ya  Lipuli katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Ilulu, mjini Lindi.

Taarifa ambazo BINGWA limezipata ndani ya Azam FC zinasema Ndayiragije amepata kibarua hicho baada ya kuwashinda makocha zaidi ya 12 walioomba kazi.

“Zimepokelewa CV zaidi ya 12 za makocha walioomba kazi, wakiwamo akina Goran Kopunovic na  Pierre Lechantre waliowahi kuinoa Simba pamoja na Aristica Cioaba ambaye aliomba kurejea tena kufundisha Azam FC,” kilisema chanzo hicho.

“Lakini pamoja na hatua zote za awali za kumpa mkataba Ndayiragije kukamilika,  Azam FC hawawezi kumtangaza hivi sasa kwa sababu bado ni mwajiriwa wa timu ya KMC,” kiliongeza chanzo hicho.

“Ndayiragije atafanya kazi ya kufundisha akisaidiana na Idi Cheche, huku Meja Mstaafu Abdull Mingange akirejea kwenye kikosi cha vijana.”

Share.

About Author

Leave A Reply