Friday, August 23

NAHODHA LIVER AGOMA KUMFANISHA SALAH NA SUAREZ – Bingwa

0


LONDON,England

NAHODHA  wa Liverpool, Jordan Henderson amekataa kumfanisha staa wa sasa wa timu hiyo, Mohamed Salahna wa zamani Luiz Suares akisema kwamba hapaswi kuulizwa swali kama hilo.

Juzi Salah alifunga mabaoa manne katika ushindi wa 5-1 dhidi ya  Watford  katika mchezo wa Ligi Kuu England  ambao umewafanya kuchupa hadi nafasi ya tatu.

Henderson  aliwahi kucheza na  Suarez  katika kipindi ambayo nyota huyo wa  Uruguay  kilikuwa chini ya  Brendan Rodgers msimu wa  2013-14 ana akweza kufunga manne katika ushindi wa  5-1 waliupata dhidi ya  Norwich City na hivyo kuonekama Salah yupo sawa na staa huyo.

Hata hivyo alipoulizwa kama wawili hao wanalingana kwa ubora, staa huyo aligoma kusema chochote zaidi ya kudaia kuwa hapaswi kuulizwa swali hilo.

“Nani ni bora kati ya wawili hawa? Upaswi kuniuliza swali  kama hili ,” Henderson alichomoa wakati alipotakiwa kutoa maoni kuhusu ni yupo mkali kati ya wawili hawa.

“Wote ni wachezaji wazuri na huwezi kuwalinganisha. Ni wachezaji wa aina tofauti.Ninachokifahamu wote wameshafunga mabao mengi na wote wanajituma uwanjani, lakini  ni vigumu kujibu swali kama hili na kila mmoja ana ubora wake,”aliongeza staa huyo.

Alisema, Suarez  tangu alihamia Barcelona  na amekuwa akifanya makubwa  na ni mchezaji ambaye ana manufaa makubwa ukicheza naye, lakini msimu huu Salah  naye amekuwa ni mchezaji wa aina yake.

The post NAHODHA LIVER AGOMA KUMFANISHA SALAH NA SUAREZ appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.