Sunday, April 21

Mtu wa soka hawezi kwenda mahakamani kupinga uchaguzi 

0


MZEE WA KUPASUA, kapssmo@gmail.com 0716985381

NA ONESMO KAPINGA

KWANZA
Mzee wa Kupasua anawapongeza Simba kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura
ya Algeria, katika mchezo wa makundi wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba
walitisha Bara la Afrika baada ya kuichapa timu hiyo mwishoni mwa wiki kwenye
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Ni
mwanzo mzuri kwa Simba kutokana na ushindi huo uliowafanya waongoze kundi lao
wakifuatiwa na Al Ahly walioshinda mabao 2-0 dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mzee
wa Kapasua akiwapongeza Simba kwa ushindi huo, lakini anasikitishwa na
wanachama wa Yanga wanaodai kwenda mahakama ya kawaida ya sheria kuzuia
uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika jana.

Uchaguzi
wa klabu hiyo ulipangwa kufanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi
Oysterbay, jijini Dar es Salaam, lakini ulisongezwa mbele kwa madai ya watu
wanaodaiwa ni wanachama wa Yanga kwenda kufungua kesi mahakamani kupinga
usifanyike.

Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Malangwe Mchungahela, walipata taarifa ya kuwapo kwa kesi mahakamani
kupinga uchaguzi huo, huku wagombea wakiwa wanaendelea na kujinadi kwa
wanachama wa klabu hiyo.

Kesi
hizo zimefunguliwa na baadhi ya wanachama kutoka mikoa ya Dar es Salaam,
Dodoma, Mbeya na Morogoro, hivyo kamati imeona haitaki kugongana na mhimili wa
mahakama.

Binafsi
naamini mtu yeyote aliyevuja jacho kucheza soka hawezi kwenda mahakamani
kufungua kesi kupinga uchaguzi usifanyike.

Watu
wanaofanya hivyo hawakucheza mpira na wanafanya hivyo kwa maslahi binafsi, baada
ya kushindwa kupata mafanikio katika nyanja nyingine.

Ninaamini
mtu aliyecheza mpira atazeeka na nidhamu yake aliyolelewa wakati akitumikia
klabu yake.

Lakini
kama atakuwa ameonewa katika jambo lolote atatafuta haki yake kwa utaratibu
uliowekwa na vyombo vya soka na si vinginevyo.

Watu
wengi wanaokimbilia mahakamani kudai haki wengi wao hawakucheza soka katika
ngazi zote.

Hao
ndio wanaosumbua katika soka, wanafikiri hawawezi kufanya kazi nyingine zaidi
ya kuwa kiongozi wa mpira wa miguu.

Ukichunguza
watu wanaopeleka masuala ya mpira mahakamani ni wale wale waliongia kwenye soka
wakiwa na malengo ya kujinufaisha kimapato.

Leo
hii tukifanya uchunguzi, waliokwenda mahakamani kuzuia uchaguzi wa Yanga
pengine ni watu waliotumwa kufanya hiyvo, nyuma yao kukiwa na mafisadi wakubwa
ambao hawataki kuona klabu hiyo ikipata maendeleo.

Isitoshe
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), limeweka wazi na kukataza masuala ya
soka kupelekwa mahakamani, bali kama kuna tatizo lolote linalohusu soka lipelekwe
katika vyombo husika vinavyoshughulikia masuala ya soka na si vinginevyo.

Kama
nilivyosema mtu wa mpira hawezi kwenda mahakamani kupinga jambo linalohusu
maendeleo ya soka katika klabu yake.

Lakini
watu waliokwenda kufungua kesi kupinga uchaguzi wa Yanga, wafahamu wengine
walijaribu kufanya hivyo lakini walishindwa na mwisho wa siku uchaguzi
ulifanyika.

Share.

About Author

Leave A Reply