Wednesday, August 21

Msiba wachelewesha dili la kiungo mpya Man United 

0


MANCHESTER, England

WINGA ambaye anakaribia kutua katika klabu ya  Manchester United,,Daniel James amepata pigo la kufiwa na  baba yake mzazi.

Kifo hicho kilitokea ikiwa ni siku chache dili hilo kukamilika akitokea Swansea City, ambapo atauzwa kwa kitita cha pauni milioni 15.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo ziliripoti kuwa usajili huo utachelewa kidogo, kutokana na msiba mzito aliopata nyota huyo.

Kifo hicho kilitokea ghafla baada ya kuugua kwa muda mfupi akiwa na umri wa miaka 60.

Share.

About Author

Leave A Reply