Saturday, May 25

Mourinho atajwa Man United

0


MANCHESTER, England

JINA la Jose Mourinho limeibukia Old Trafford kama utani na hiyo ni baada ya kiungo anayesepa zake, Ander Herrera, kusema kocha huyo hakuwa tatizo wakati timu hiyo ilipokuwa ikifanya vibaya.

Kwa anavyoona yeye, wachezaji wanapaswa kubebeshwa lawama kwa asilimia 75 ya kile kilichoikuta Man United, hata kugharimu kibarua cha mkufunzi huyo.

Herrera aliongeza kuwa Mourinho raia wa Ureno alifanya kila linalowezekana kukiokoa kikosi hicho lakini wachezaji hawakutekeleza majukumu yao.

“Sote tunatakiwa kubeba lawama. Si sawa kulaumu wengine. Unapokuwa na msimu mbaya, asilimia 75 ni jukumu la wachezaji,” alisema Herrera.

“Ni rahisi sana kocha anapoondoka kuanza kulaumu wengine lakini ni kosa la kila mmoja.”

Share.

About Author

Leave A Reply