Sunday, August 18

MORATA ‘OUT’ HISPANIA – Bingwa

0


LONDON, England

STAA wa Chelsea, Alvaro Morata, ameachwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Hipania kitakachomenyana na Argentina na Brazil.

Morata amekuwa katika kiwango kisichoridhisha akiwa na klabu yake Chelsea, hivyo kushindwa kumshawishi kocha wa Hispania, Julen Lopetegui.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lobetengui alisema Morata si sehemu ya mipango yake katika mechi za kirafiki za hivi karibuni.

Lakini, kocha huyo aliongeza kuwa Morata ana nafasi ya kucheza Kombe la Dunia.

“Na uhakika tutamtumia. Anayo nafasi, tutamwangalia hadi msimu utakapokwisha na tutakuwa naye.

“Sina shaka juu ya hilo, ni mchezaji mwenye umri mdogo na bado ana kitu,” alisema Lobengetui.

The post MORATA ‘OUT’ HISPANIA appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.