Thursday, August 22

Minziro njia panda Singida United

0


NA WINFRIDA MTOI

KOCHA wa Singida United, Fred Minziro, amesema bado hajafahamu hatima yake, kuendelea kukinoa kikosi hicho kwa msimu ujao kwa kuwa mkataba wake unamalizika mwezi huu. Akizungumza na BINGWA jana, Minziro, alisema yeye aliitwa na uongozi wa Singida United kwa lengo la kuisaidia timu hiyo baada ya makocha waliokuwepo kuondoka.

Alisema hadi sasa hawajafanya mazungumzo yoyote na uongozi wa timu kuhusu mkataba mpya, lakini ikitokea yupo tayari kuendelea kubaki kikosini hapo.

“Mkataba wangu na Singida unamalizika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu, kwa sababu ndiyo makubaliano yetu ikitokea wakaniongezea sawa nipo tayari, ila ninachoangalia kwa sasa ni kuhakikisha timu inaendelea kuwepo katika ligi,” alisema Minziro.

Akizungumzia mchezo wake wa mwisho na Coastal Union, alisema anakwenda kupambana akijua  dimba la Mkwakwani ni gumu. “Kwa pointi tulizonazo tumeshaondoka katika hatari ya kushuka daraja, ila tunahitaji ushindi mbele ya Coastal Union, ili kumaliza ligi kwa heshima,”

alisema Minziro. Katika msimamo wa ligi hiyo, Singida ipo nafasi ya 11 na pointi 45, baada ya kucheza michezo 37, imeshinda 11, sare 12 na kupoteza 14.

Share.

About Author

Leave A Reply