Sunday, August 25

Michuano ya kimataifa karate kufanyika Julai

0


NA MWANDISHI WETU

TANZANIA
inatarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano ya kimataifa ya karate iliyopangwa  kufanyika Julai mwaka huu jijini Dar es
Salaam, ikishirikisha Bara la Afrika na Asia.

Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari juzi na Mkufunzi Mkuu wa
Karate Tawi la Tanzania, Jorome Mhagama, michuano hiyo imeandaliwa kwa lengo la
kujenga urafiki na uhusiano.

Taarifa
hiyo ilisema lengo jingine la michuano hiyo ni kutoa nafasi kwa wachezaji
kujifunza katika nchi husika.

Ilisema
ni faraja kwa viongozi wa chama cha karate nchini kupata nafasi ya kuandaa
michuano hiyo, jambo ambalo anaamini litalitangaza Taifa ndani ya Afrika na dunia
kwa ujmla.

Katika
michuano hiyo, pia kutakuwa na semina na mtihani  wa nadharia na vitendo.

Share.

About Author

Leave A Reply