Sunday, August 25

Mgunda ataka usajili ‘bab kubwa’

0


ZAINAB IDDY

KOCHA wa timu ya Coastal Union ya jijini Tanga,
Juma Mgunda, amesema kuwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara anahitaji kuwa
na kikosi kipana na cha ushindani ili kuepukana na changamoto alizokutana nazo 2018/19.

Katika msimu huu uliofika tamati wiki hii,
Coastal Union imemaliza ikiwa katika nafasi ya nane, ikiwa na alama 48
ilizozipata ndani ya mechi 38.

Akizungumza na BINGWA jana, Mgunda alisema msimu huu
amefanikiwa kutimiza malengo ya kuibakiza timu katika ligi hiyo, lakini ujao
mipango ya uongozi ni kuiwezesha kumaliza ndani ya nne bora.

“Nashukuru Mungu msimu huu nimetimiza malengo
tuliyoyaweka na viongozi mara baada ya kupanda ligi kwa kuibakiza timu, lakini
msimu unaokuja, lazima tuvuke malengo ya sasa.

“Katika ripoti yangu nitakayoikabidhi nitahitaji
ufanyike usajili wa uhakika ambao utakuja kutupa kile wanachohitaji wadau wa
Coastal Union,” alisema.

Aliongeza: “Sitokuwa tayari kuona ninaifundisha
timu yenye wachezaji wengi wasio na viwango, nataka kila tutakayecheza naye,
aondoke na kumbukumbu ya kupoteza mbele yetu.”

Share.

About Author

Leave A Reply