Tuesday, August 20

Meneja wa Samatta kuwapa shavu wachezaji kibao

0


NA WINFRIDA MTOI

MENEJA wa mshambualiaji wa Kimataifa wa Tanzania,
Mbwana Samatta, Jamal Kisongo, ameingia sokoni kusaka klabu za kuwapeleka
wachezaji wake walioonekana kufanya vizuri msimu huu katika Ligi Kuu Tanzania
Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Kisongo, alisema ana
wachezaji wengi anaowamiliki katika klabu za hapa nchini, lakini kutokana na
Ligi Kuu kukosa mdhamini soko la Tanzania limekuwa gumu.

Alisema kwa hali hiyo ameona kuna haja ya kujaribu
kuwatafutia timu za nje wachezaji wake, hasa wale wanaoonekana kufanya vizuri
ili wakaendeleze vipaji vyao.

Kisongo alisema kitendo cha Ligi Kuu kukosa mdhamini
kinawafanya wachezaji wengi kuishi katika mazingira magumu kwa kuwa hawalipwi
mishahara kwa wakati unaotakiwa, hali inayosababisha washindwe kufanya kazi
kiufanisi.

“Tayari kuna baadhi ya wachezaji nimeshawapatia
timu, mazungumzo yanaendelea vizuri, ninachosubiri ni dirisha la usajili
lifunguliwe hasa kwa wale wanaomaliza mikataba itakuwa ni rahisi.

“Ninafanya hivyo kwa kuwa ninachohitaji ni kuona
wachezaji wangu wanapiga hatua na kufanya kazi katika mazingira mazuri, kila
mmoja aweze kunufaika,” alisema Kisongo.

Kisongo aliwataja baadhi ya wachezaji wake
walioonyesha viwango vizuri na timu zao na yupo katika mchakato wa kuwapeleka
nje kuwa ni Ayoub Lyanga, Haji Ugando (Coastal Union) na Haruna Chanongo
(Mtibwa Sugar).

Share.

About Author

Leave A Reply