Thursday, August 22

MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU ISCO – Bingwa

0


LONDON, England

JINA la Isco limekuwa gumzo barani Ulaya baada ya ‘hat trick’ yake kuimaliza Argentina mbele ya Hispania.

Katika mtanange huo wa kirafiki uliochezwa mjini Madrid, Hispania, wenyeji walishinda mabao 6-1.

Timu hizo zinajiandaa na fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 14 nchini Urusi.

Hata hivyo, Isco anazungumziwa zaidi kwa kuwa amekuwa akikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha Real Madrid kwani msimu huu, ameingia ‘first eleven’ mara 25 pekee.

Je, ni nani huyo? Makala haya yanakuletea mambo 10 ambayo huenda hukuyajua kuhusu kiungo huyo.

  1. Mashabiki wa Madrid watakumbuka kuwa Agosti 18, 2013, Isco alifunga na kutoa ‘asisti’ katika mechi yake ya kwanza akiwa na timu hiyo. Ulikuwa ni mchezo wa La Liga dhidi ya Real Betis.
  2. Mwanasoka huyo anatoka na mwanamitindo Carmen Munoz. Alianza uhusiano na mlimbwende huyo baada ya kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu, Victoria Calderon, ambaye ndiye mama wa mwanawe, Francisco Jr.
  3. Jarida la Forbes linamtaja Isco kuwa na utajiri wa Dola za Marekani milioni 12, zaidi ya Sh bilioni 120 za Tanzania. Nyota huyo anavuna mshahara wa Dola milioni 4 kwa mwaka pale Madrid.
  4. Mkali huyo aliwahi kutajwa ‘kuchepuka’ na mwanamuziki Rihanna. Taarifa hizo zilishika kasi baada ya mrembo huyo kuonekana Hispania, ikielezwa kuwa alikuwa na Isco katika moja ya mitoko yake.
  5. Baba yake mzazi, Paco Alarcon, alikuwa mfanyakazi wa hoteli wakati Isco akiwa mdogo. Hata hivyo, mzee huyo ameshaikacha kazi hiyo na sasa ni wakala wa mwanawe.
  6. Kama ilivyokuwa kwa Jack Wilshere, Isco alizaliwa akiwa na matege. Mbali na hiyo, pia alikuwa kibonge. Licha ya hali hiyo, bado alipambana kuzifikia ndoto zake za kuwa mwanasoka na sasa ni staa.
  7. Kwa mujibu wa mtandao wa ESPN, Isco alikaribia kutua Manchester United lakini timu hiyo ilimkataa kwa kuwa alikuwa na kichwa kikubwa. Kipindi hicho, staa huyo alikuwa Malaga.
  8. Kama atakwenda Urusi wakati wa majira ya kiangazi, basi hizo zitakuwa ni fainali zake za kwanza za Kombe la Dunia. Hajawahi kucheza michuano hiyo, wala ile ya Euro.
  9. Isco ana mbwa wake ambaye ameamua kumwita Messi. Wakati anajiunga na Madrid, alisema kuwa aliamua kumpa jina hilo kutokana na ubora alionao Muargentina huyo.
  10. Jamaa ni shabiki mkubwa wa Valencia, klabu iliyoibua kipaji chake kupitia ‘academy’ yao kabla ya kumuuza Malaga ambayo ndiyo iliyompeleka Madrid.

The post MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU ISCO appeared first on Bingwa.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.